Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi; Fidelica Myovella Wamefanya Kikao Cha Kamati ya Lishe kwa kipindi Cha robo ya Nne kuanzia April Hadi June kwa Mwaka wa Fedha 2024-2025.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi; Fidelica Myovella amesema Wahudumu wa Afya na Wazazi Wajitahidi kutoa Huduma ya Lishe Bora kwa Watoto Wanapokuwa Shuleni au Nyumbani ili kuepuka Utapia mlo ambao unaweza kuleta athari ya udumavu wa Akili kwa Watoto.
"Wazazi ambao ni Wajawazito wafuatiliwe vizuri na Wahudumu wa Afya kwa kupewa Huduma nzuri za Lishe ukizingatia Mkoa Wa Iringa Umebarikiwa upatikanaji wa Vyakula vingi hivyo inakuwa rahisi kwa Wajawazito kupata urahisi wa kupata hivyo Vyakula vya Lishe,pia Wazazi wote Wazingatie Matumizi ya Lishe Bora kwa Watoto ili kupata Vizazi Bora vyenye Werevu." Amesema.
Naye Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Peter Ngusa amesema Wakuu wa Shule Wajitahidi Kuzingatia Lishe Bora kwa Wanafunzi ili kusaidia kupata Elimu Bora pia Wazazi Wajitahidi kupanda Mboga mboga katika Mazingira ya Nyumbani ili kurahisisha Upatikanaji wa Lishe Bora.
Vedasto Faustine Malima
Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.