“Hakikisheni wananchi tulio wahamasisha kujiandikisha katika Orodha ya wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sasa tunawahamasisha wakapige kura tarehe 27 Novemba 2024 na kufanya uchaguzi wa Amani kwa kuzingatia 4 R za Mheshimiwa Rais.
Tuhakikishe wananchi tuliowaandikisha wanajitokeza kupiga kura tarehe 27 Novemba 2024 , ili wapate haki ya kuchagua viongozi wanaowataka ili kuweza kupanga mipango yao ya Mitaa kwa ushirikiano.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa alipokuwa akizungumza kwenye
Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupitia taarifa za Robo ya kwanza Julai - Septemba 2024/2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kuendelea kufanya vizuri katika sekta mbalimbali huku akiiangazia Sekta ya Michezo na Utamqduni ambayo katika Michezo ya SHIMISEMITA 2024 Imefanikiwa kushinda, ngoma Mshindi wa kwanza, Mpira wa wavu wasichana mshindi wa kwanza na Nishani ya Kurusha Tufe mshindi wa kwanza kwa Neema Chongolo
“Ili upate mabadiliko lazima ufanye tofauti ,tuache mazoea katika utekelezaji wa majukumu yetu. Lazima tufikiri tofauti
Tukiacha mazoea hakuna atakayeifikia Halmashauri ya Mji Mafinga” Dc Mufindi Dkt Linda Salekwa.
Amesema Mwaka 2024 Halmashauri ya Mji Mafinga imeshika nafasi ya kwanza Kitaifa kanda ya pili katika Mbio za Mwemge
Wa Uhuru 2024 ambapo Halmashauri imekabidhiwa Kombe la Ushindi, Cheti na fedha shilingi milioni 1
Imeandaliwa na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Picha za matukio mbalimbali za Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt Linda Selekwa akizungumza na madiwani na Wakuu wa Idara na Vitengo katika Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.