Leo Tarehe 3/4/2024 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa ameitisha kikao cha kwanza cha Maandalizi ya Mbio za Mwenge 2024 ambapo Mkoa wa Iringa unategemea kupokea Mwenge wa Uhuru 2024 Tarehe 22/6/2024 kutoka Mkoa wa Njombe na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inategemea kupokea Mwenge tarehe hiyo.
Halmashauri ya Mji Mafinga inategemea kupokea Mwenge tarehe 25/6/2024 na utakabidhiwa tarehe 26/6/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Aidha Mkuu wa Wilaya amezitaka Halmashauri zote Mbili za Wilaya ya Mufindi kuhakikisha Miradi iliyopendekezwa ikamilike Kama haijakamilika na taarifa za Miradi yote zipitiwe na kukaguliwa kabla ya Mwenge Kufika.
Dkt Linda Salekwa amewataka Wakuu wa Taasisi zote, Wananchi na Watumishi kuhakikisha wanafanya Maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru 2024 sehemu zote utakapopita kwani Mwenge unaleta na kuchachua Maendeleo ikiwa ni pamoja na kukamilisha Miradi, kufichua wala rushwa na kusambaza jumbe mbalimbali za Kitaifa.
Akitoa taarifa ya Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mji, Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mji Mafinga Ndugu Henry Kapella amesema Mwenge Utakesha katika uwanja wa Mashujaa Katikati ya Mji wa Mafinga.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Usalama Wilaya ya Mufindi, Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya ya Mufindi, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi mbalimbali, Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri mbili za Wilaya ya Mufindi.
Imeandaliwa na
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.