“Zoezi la kusafisha Dampo hufanyika kwa lengo kuweka mazingira ya eneo la kutupa taka kuwa katika utaratibu mzuri kwa Afya ya watumiaji wa Eneo hilo na Mji kwa ujumla ambapo zoezi hili hufanyika kila baada ya miaka 2 au 3.”
Akizungumza Mkuu wa Kitengo Cha Usafi wa Mazingira na Udhibiti wa Taka Ndugu, Charles Tuyi amesema ni utaratibu wa Kawaida kwa Halmashauri kusafisha Dampo
kwaajili ya kukusanya taka eneo moja na kutoa urahisi kwa magari kuingia kutupa taka hizo.
Naye Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella akizungumza akiwa aneo la Dampo amesema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha Mji unaendelea kuwa safi na kuwaomba wananchi kuchangia ushuru wa Taka wanapotakiwa kufanya hivyo. Aidha amewaomba wananchi wanaochukua chupa tupu na taka nyingine kutoka dampo na kurudisha kwenye jamii kuwa makini na matumizi ya bidhaa hizo kwa Afya zao na jamii inayowazunguka.
Eneo la kutupa taka lina jumla ya Ekari 57 ambapo Ekari 15 zimetengwa kwaajili ya Maji Taka na Ekari 42 ni eneo la Dampo.
Imeandaliwa na
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.