“Jumla ya Viwanja 2618 vimepimwa na vinaandaliwa Umiliki kwa Kata ya Upendo na Kinyanambo ambapo mwananchi anakuja na kuandaliwa Hati yake hapa na ikishakamilika ataitwa na kukabidhiwa lengo la Clinic hii ya Ardhi ni kuwafuata wananchi walipo na kuwapa huduma za Ardhi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zote za Ardhi katika Mji Mafinga”
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Iringa Bi, Rehema Kilonzi alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi kwenyezoezi la Clinic ya Ardhi katika Kata ya Upendo ndani ya Halmashauri ya Mji Mafinga.
Bi. Rehema amesema mpaka sasa jumla ya wananchi 341 wamehudumiwa ikiwa ni siku ya pili ya Clinic hii na viwanja 7445 vimepangwa kupimwa katika kata ya Upendo na Kinyanambo katika Halmashauri ya Mji Mafinga
Nae Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Geofrey Kabuje amesema muitikio ni mkubwa sana , hivyo zoezi hili litakuwa ni endelevu katika Kata zote. Amesema huduma zinazotolewa ni pamoja na Kutayarishiwa Hati Miliki, Kupokea, kusikiliza na kutatua Migogoro ya Ardhi, Kutoa Ushauri wa Masuala mbalimbali ya Ardhi, Kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi na kutoa Elimu juu ya Sheria za Ardhi.
“nimetumia dk 20 kuanzia, kupokelewa, kupatiwa bili ya malipo, kuandaliwa nyaraka hadi kusaini hati yangu.* nimepigiwa tu simu nije hapa hata sikudhani kama itakuwa haraka hivi nimeshangaa kweli Serikali imejipanga natamani hii huduma itolewe kata zote yaani nimehudumiwa vizuri naishukuru Serikali kwa kuamua kuwafuata wananchi hadi ngazi ya Kata na kutoa huduma za Ardhi” Amesema mwananchi aliyenufaika na huduma ya clinic ya Ardhi Kutoka kata ya Upendo Godfrey Mduda
Na Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano
Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.