Zaidi ya wananchi 139 katika Halmashauri ya Mji Mafinga hususan katika Kata ya Upendo wamepatiwa huduma katika Clinic ya Ardhi Halmashauri ya Mji Mafinga.
Akizungumza Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Geofrey Kabuje kwa Niaba ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Iringa Bi Rehema Kilonzi amesema kuwa, ikiwa leo ni siku ya kwanza ya kutoa huduma hii muitikio umekuwa mkubwa sana ambapo jumla ya wananchi 139 wamepatiwa huduma ikiwemo huduma ya Kutayarishiwa Hati Miliki, Kupokea, kusikiliza na kutatua Migogoro ya Ardhi, Kutoa Ushauri wa Masuala mbalimbali ya Ardhi, Kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi na kutoa Elimu juu ya Sheria za Ardhi.
Kabuje amesema zoezi la Clinic ya Ardhi katika Kata ya Upendo litafanyika kwa muda wa siku 6 kuanzia saa 2.30 Asubuhi mpaka saa 10.00 Jioni katika Ofisi ya Kata ya Upendo na zoezi linaendelea na litakuwa Endelevu kwa kata zote lengo likiwa kuhakikisha natatizo na changamoto za Ardhi zinatatuliwa na wananchi wanapata huduma za Ardhi kwa wakati
Na Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.