Halmashauri ya Mji wa Mafinga imepongezwa kwa kukusanya mapato kwa asilimia 28 kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 kauli hiyo imesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Regnant Kivinge katika Baraza la Madiwani ambalo limefanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri.
Mheshimiwa Kivinge ametoa pongezi hizo kwa Mkurugenzi pamoja na watumishi wote wa Halmashauri kwa kuendelea kukusanya mapato ambayo yanasaidia kuendesha halmashauri na kusaidia kutatua kero za wananchi katika maeneo yao sambamba na hilo ametoa rai kwa watumishi kuongeza kasi ya ukasanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo.
Aidha katika Baraza la Halmashauri Mheshimiwa Charles Makoga Diwani wa Kata ya Isalavanu ameshauri kuanzisha shule maalumu kwa ajili ya michezo kwani kwa sasa michezo ni ajira hivyo itasaidia vijana wengi kujiajiri kupitia michezo ambayo itasaidia kukuza vipaji vyao na kujipatia kipato kupitia michezo .
Kwa upande mwingine Halmashauri ya Mji wa Mafinga imepongezwa na Baraza la Madiwani kwa kundelea kufanya vizuri katika mshindano na michezo mbalimbali ambayo yanajumuisha Halmashauri mbalimbali ikiwemo Shimisemita ambapo Halmashauri imeibuka na ushindi wa makombe matatu ambapo katika mpira wa wavu ilishinda nafasi ya kwanza , kwaya nafasi ya tatu, na katika ngoma imeshinda mshindi wa kwanza. Halmashauri ya mji mafinga pia imepongezwa kwa kushindi wa nafasi ya kwanza Kanda ya pili katika mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri amempongeza Mkurungenzi Bi.Fidelica Myovela pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo kwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na kuhakikisha Halmashauri inasonga mbele na pia kuwaletea wananchi maendeleo na kutatua kero zao katika maeneo yao.
Imetolewana Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mji Mafinga
Michael Ngowi
Picha za matukio mbalimbali katika Baraza la madiwani ambalo limefanyika leo Halmashauri ya Mji Mafinga.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.