Halmashauri ya Mji wa Mafinga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imetoa elimu ya mikopo ya asilimia kumi katika Kata ya Bumilayinga baada ya mikopo hiyo kurudishwa ambapo wanafuaika wa mikopo hiyo ni makundi ya vijana, wanawake pamoja na walemavu ambapo Halmashauri ya Mji wa Mafinga imetenga jumla ya shilingi Bilioni 1.6.
Elimu hiyo imetolewa katika mitaa ya Bumilayinga, Matanana, Urole, Kisada, Weru, Ibikititu na Mtula ambapo wananchi wa maeneo hayo wamepewa elimu juu ya kuunda vikundi vinavyo kizi masharti ikiwemo, kuwa na katiba ya kikundi, vitambulisho vya nida kwa kila mwanachama wa kikundi, barua za utambulisho kutoka serikali za mitaa au vijiji pia kikundi kiwe na andiko la mradi unao tekelezeka na kikundi kiwe na akaunti ya benki.
Aidha Diwani wa Kata ya Bumilayinga Mheshimiwa Anderson Mwakyusa amewataka vijana, wanawake pamoja na walemavu kuhakikisha wanachangamkia fursa hii ya mikopo ili iweze kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na pia mikopo kufanya marejesho na pia mikopo hii aina riba.
Pamajoa na elimu hiyo kutolewa wananchi wa Kata ya Bumilayinga wameishukuru serikali kwa kurejesha tena mikopo hiyo kwani imekuwa ikiwasaidia wananchi wengi kujikwamua kiuchumi ikiwemo makundi ya wanawake, vijana na walemavu hivyo itasaidia kukuza mitaji na vipato vyetu katika maeneo haya.
hiyo itakuwa na muda wa matazio wa miezi mitatu kabla ya kuanza.
imeandaliwa na Michaele Ngowi
Afisa Habari
Wanachi wa Mtaa wa Matanana wakisikiliza elimu ya upatikanaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa vijana ,wanawake, na watu wenye ulemavu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.