Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt linda Salekwa amesema imefika wakati wa Wazazi wahakikishe wanajibika katika malezi ya watoto kwani kwa kufanya hivo kutasaidia kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia.
" Ipo haja ya kurejea asili zetu katika familia Baba kama Baba na Mama kama Mama wakati ni sasa wakinababa kuhakikisha wanasimamia majuku yao yanayohusu familia pia wakina mama kuhakikisha wanasimamia nafasi zao kwa kufanya hivo kutapunguza matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi ameyasema hayo kwenye Maadhimisho ya familia duniani lengo likiwa ni kukumbushana umuhimu wa familia katika suala zima la maadili kwa jamii.
Nae Mkuu wa dawati la jinsia Afande Mary Haule amesema Wazazi wahakikishe wanapata muda wa kuzungumza na watoto wao kwani kufanya hivo kutapunguza matukio ya ukatili wa kijinsia na kutosita kutoa taarifa pindi watoto wanapofanyiwa matukio ya ukatili wa kijinsia na watu wao wa karibu na kuepuka kuyamaliza masuala kifamilia kwa kufanya hivo kunachochea ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema tunawajibu wakukumbushana suala la maadili katika familia zetu kwani yapo mambo yanabidi tuyakemee kama ubakaji na ulawiti haya ni mambo yanayokosesha upendo katika familia zetu.
Maadhimisho ya siku ya familia duniani yamehudhuriwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Mufindi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mufindi, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Madiwani, Wananchi na Wafanyabiashara wa soko kuu la Mafinga.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO MAFINGA - TC
Christopher Mhina
Mwandishi wa Habari Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.