Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Selakwa ameongoza kikao cha ushauri cha Wilaya (DCC) kilicho husisha Halmashauri mbili za Wilaya ya mufindi ambapo wamejadili rasimu za bajati 2025- 2026 za Halmashauri pamoja na Taasisi za TARURA na RUWASA pamoja na kupokea maoni ya wananchi na Azaki mbalimbali zisizo za kiserikali.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt Linda Selekwa amewataka Wakurugenzi kuhakikisha katika bajeti hii ya sasa ni kusimamia miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa kwa mapato ya ndani ikiwemo uboreshwaji wa kiwanja cha michezo na ambayo yatasababisha wananchi kupata huduma iliyo bora ka kwa kiwangu cha juu .
Aidha Dkt Linda Selekwa ameagiza katika bajeti ya sasa ambayo imejadiliwa ni kuhakikisha inakuwa na bajeti ya kuwaangalia wazee pamoja na makundi mengine maalumu ikiwemo walemavu, vijana na wanawake katika Wilaya yetu pia ameongeza kwa kusema Halmashauri ni lazima zisimamie ukusanyaji wa mapato ili bajeti ziweze kutekelezeka ikiwemo kutenga bajeti kwaajili ya matengenezo ya barabara.
Akiwasilisha bajeti hiyo Afisa Mipango Ndugu Peter Ngusa amesema Kwa upande wa Halmashuri ya Mji Mafinga imepanga matumizi ya makadirio ya bajeti ya 2025- 2026 kutumia kiasi cha shilingi bilioni 31.4 ambapo mapato ya ndani yanakadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 7.5 ambayo yatasaidia kuanziasha na kumilisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani.
Kwa upande wa bajeti za Taasisi za TARURA na RUWASA Dk Linda amezitaka kuchukua ushauri na maoni yanayotolewa na wananchi ili kuhakikisha na kuweza kutatua changamoto za miundombinu ikiwemo barabara za maeneo mbalimbali za Wilaya ya Mufindi ili kuweza kupitika kirahisi na kufikisha huduma kwa wananchi. Na kwa upande wa RUWASA wametakiwa kuhakikisha wanasimamia bajeti zo na kusambaza huduma ya maji na kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa maji wa miji 28 ambao unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 48 katika Mji wa Mafinga.
Michael Ngowi Afisa Habari
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.