Halmashauri ya Mji Mafinga inahakikisha watumishi wake wanafanya kazi katika mazingira yaliyoboreshwa ikiwa ni pamoja na kuwapandisha vyeo watumishi kwa wakati, kulipa madeni na kununua vitendea kazi kwaajili ya kuboresha utendaji wao, hatua hizi ni wazi zinaongeza morali kwa wafanya kazi kufanya kazi kwa bidii.
Hayo yamebainika kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la kawaida kupitia Utekelezaji wa Kazi za Halmashauri ya Mji Mafinga, Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji na kuhudhuriwa na Wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya wafanyakazi kikiwemo CWT,TUGHE, TALGU na Wakuu wa Divisheni na Vitengo .
Akisoma taarifa Ndugu Raineli Mwenda Afisa Utumishi amesema Halmashauri imekuwa ikifuata sheria na miongozo ya utendaji kazi katika kuamua masuala mbalimbali ya kazi.
Naye Ndugu Charles Mwaitege kwa niaba ua Mkurugenzi wa Mji amewataka watumishi kuendelea kufuata Sheria, kanuni na misingi ya Utumishi wa Umma jambo ambalo litaondoa migogolo yoyote katika Taasisi lilifuatwa.
Ameongeza kuwa Halmashauri ipo hatua za kukamilisha mkataba wa huduma kwa wateja ambao utakuwa ni makubaliano kati ya Halmashauri na wateja wake kuhusiana ma namna ya kutoa huduma zake.
Naye Afisa Kazi Mkoa wa Iringa Bi , Leorada Mbiki amesisitiza umuhimu wa Baraza la Wafanyakqzi kuwa ni chombo cha Juu kinachounganisha watumishi na Mwajiri hivyo ametoa pongezi
Kwa Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu. Ayoub Kambi kwa kufuata taratibu na Sheria za Serikali za Mitaa katika Utendaji kazi na lusimamia haki za watumishi.
Halmashauri ya Mji Mafinga inajumla ya watumishi 1177 kupitia Divisheni 9 vitengo 9 na vituo vya kazi 155.
Imetolewa na Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.