MKURUGENZI MJI MAFINGA AWAPA MIKAKATI ASKARI MGAMBO YA UKUSANYAJI WA MAPATO.
“ Kazi yoyote inayogusa maisha ya wananchi hakikisheni mnaifanya kwa busara sana na si kutumia nguvu, hii itajenga mahusiano mazuri kati na wananchi na Serikali kwani wananchi ndio walipa kodi na ushuru mbalimbali wa Halmashauri”
Kauli hiyo imesemwa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer alipokuwa akizungumza na Askari Mgambo wa Halmashauri ya Mji Mafinga lengo likiwa ni kuwapa mikakati ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Amesema kila mtu kwenye nafasi yake lazima atimize wajibu wake na ahakikishe katika kutekeleza wajibu wake busara inawaongoza kuliko nguvu hii ni katika kujenga mahusiano mazuri na wananchi, na kila mtu kwenye eneo lake alilopangiwa ahakikishe anayetakiwa kulipa ushuru wa Halmashauri alipe ushuru huo.
Aidha Mkurugenzi aliweza kusikiliza changamoto za Askari Mgambo hao na kuwaahidi kutatua changamoto zinazowakabili katika Utendaji wao wa Kazi na kuwataka kufanya kazi kwa Kufuata Kanuni, Sheria na Maadili ya Utumishi.
Kikao cha Mikakati ya Mapato Kimehudhuriwa na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Mji Mafinga pamoja na Askari Mgambo wanaohusika kwenye Maeneo ya Ukusanyaji wa Mapato.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.