Katika kuhakikisha wananchi wanafanya biashara katika mazingira wezeshi na kujali Afya za walaji Halmashauri ya Mji Mafinga imejenga machinjio ya Nguruwe katika Kata ya Changarawe itakayowezesha wafanyabiashara kuchinja mifugo sehemu salama na kupimwa na madaktari ili kuhakikisha afya za walaji na maeneo ya uchinjaji huku Halmashauri ikikusanya Ushuru kwaajili ya kuendelea kuboresha huduma nyingine kwa wananchi”
Akizungumza Mkurugenzi Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella amesema machinjio ya Nguruwe imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 43.7 kutoka Mapato ya ndani ambapo lengo la Serikali ni kuona wafanyabiashara wanafanya biashara katika maeneo rafiki yanayowawezesha kutoa huduma bora kwa jamii, hivyo machinjio inaendelea kuboreshwa miundombinu ya nje
Akizungumza Daktari wa Mifugo Mji Mafinga Aldonis Ulimboka amesema maji tayari yapo ya kutosha katika machinjio hiyo na tenki la kuhifadhia maji yakikatika lipo hivyo wakati ukifika wafanyabiashara hao watatakiwa kuja kuanza shughuli zao katika machinjio hiyo iliyopo Kata ya Changarawe.
“ kuweka machinjio katika eneo moja inazuia uchinjaji holela mitaani ambapo mtu anaweza kuchinja bila nyama hiyo kukaguliwa na akaisambaza kwa walaji na kuhatarisha Afya za watumiaji lakini hapa itapimwa na madaktari na ubora wa nyama utakuwa wa kutosha na mazingira ya kuchinjia yatakuwa salama
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.