Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Bi Fidelica Myovella leo tarehe 30 Disemba 2024 ameboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la Mpigakura katika kituo cha Ivambinungu katika kata ya Boma kufuatia zoezi la Kitaifa linaloendelea la Uandikishaji wa Wapiga Kura.
Kupitia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Uboreshaji wa Daftari katika Mkoa wa Iringa, Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwawa ulianza tarehe 27 Disemba na Unatarajiwa kumalizika tarehe 2 Fedruary 2024.
“Mimi nimeboresha taarifa zangu, wewe je” niwahimize wananchi ambao hamjajitokeza kuja kujiandikisha na kuboresha taarifa zao” kujiandikisha ni haki yako”
TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovella akiboresha taarifa zaka katika daftari la kudumu la mpiga kura .
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.