MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI MAFINGA AHESABIWA TAREHE 23/8/2022 NA KUENDELEA KUWAOMBA WANANCHI WA MAFINGA NA TAIFA KWA UJUMLA KUTOA USHIRIKIANO PALE TU WATAKAPOFIKIWA NA KARANI WA SENSA ILI KUHAKIKISHA SENSA INAFANIKIWA KWA MAENDELEO YA TAIFA LA TANZANIA.
“ Wananchi wa Mji Mafinga na Tanzania kwa ujumla zoezi hili limeanza Rasmi leo tarehe 23/8/2022 na kama alivyosema Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa nchi yetu ni kubwa sana, hivyo zoezi hili litaendelea kwa muda wa siku saba, na kama hujahesabiwa tarehe 23/8 hakikisha siku ukifikiwa na Karani wa SENSA utoe ushirikiano na taarifa za kuamkia tarehe 23/8 na si vinginevyo”
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi,Happiness Laizer baada ya kuhesabiwa nyumbani kwake Mafinga, Mtaa wa Ivambinungu kata ya Boma.
Amesema zoezi hili ni muhimu katika Mipango Endelevu ya Nchi kwani mipango yote ya sekta mbalimbalimba za Elimu, Ujenzi, Uchumi, Afya, Ustawi wa jamii, kilimo na mingine inapangwa kutokana na SENSA ya watu na makazi ambapo kwa Tanzania zoezi hili hufanyika kila baada ya miaka kumi na kuwezesha Serikali kutambua idadi ya watu wake ili kurahisisha kupanga mipango ya nchi.
Zoezi la kuhesabiwa Mkurugenzi wa Mji Mafinga limefanywa na karani wa SENSA Erick Haonga.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.