Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama(W) amefanya ziara ya kukagua Njia na Miradi itakayopitiwa /kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2025 ambao unatarajiwa kukimbizwa katika Halmashauri ya Mji Mafinga Tarehe 1/5/2025.
Kamati hiyo imeshauri na kuboresha baadhi ya Miradi ili chamgamoto zilizoonekana kwenye baadhi ya Miradi zifanyiwe kazi ili kuweza kukidhi vigezo vya mwenge kwa mwaka 2025 na kuhakikisha ushindi unapatikana.
Miradi iliyopitiwa ni Mradi wa wodi daraja la kwanza, utunzaji wa mazingira sokoni, nishati safi pandamiti kibiashara, ofisi ya Kata kinyanambo, barabara, Maji , bweni la watoto wenye mahitaji maalumu shule ya Msingi Amani.
Ushauri la kuboresha ulipokelewa na Timu ya Menejimenti ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Ndugu Charlles Mwaitege.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.