MWENGE WA UHURU 2024 WAZINDUA MIRADI 9 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.1 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
Halmashauri ya Mafinga Mjini imeupokea Mwenge wa Uhuru leo tarehe 23/06/2024
na jumla ya miradi 9 ya Maendeleo imepitiwa na Mwenge huo.
Akiupokea Mwenge katikq Viwanja vya Shule ya Msingi Wambi, Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amesema Mwenge wa Uhuru utapita katika Miradi 9 ya Maendeleo ambayo ipo katika kata 5 kati ya 9 na utakimbizwa kilometa 49.9.
Mwenge wa Uhuru 2024 umekagua shughuli za kuwawezesha wanafunzi wenye mahitaji Maalumu katika Shule ya Msingi Makalala Katika ukaguzi huo Mkimbiza Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amekabidhi viti mwendo viwili (2) kwa watoto wenye uhitaji vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi ili kuwasaidia watoto wenye uhitaji.
Katika hatua nyingine Mnzava amesema kutokana na mauaji yaliyotokea ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ameagiza kamati za usalama wilaya zote kuwalinda watoto wenye ulemavu wa ngozi na kuwatambua kwa idadi kupitia kupitia maafisa ustawi wa jamii.
Kwani nao wana haki ya kulindwa kama watu wengine na hili limedhihirishwa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto hao wenye uhitaji Maalumu.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.