“ Sisi tunaoanzisha michakato ya manunuzi tunalalamikiwa hatulipi wazabuni kwa wakati Kulingana na makubaliano ya mkataba na kupelekea kuathiri wazanuni kushindwa kuendelea kufanya kazi kwenye Taasisi nyingine na wanashindwa kulipa kodi .hii ni changamoto kubwa. Tukumbuke ni takwa la kisheria kulipa wazabuni kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa na Ndugu Paschael Monono Meneja wa Kanda PPRA Nyanda za Juu Kusini alipokuwa akifungua mafunzo
Ya kuwajengea uwezo watumiaji wa Mfumo wa Manunuzi NeST katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Amesema kama watendaji tunatakiwa kutekeleza wajibu wetu kuhakikisha wazabuni wanalipwa kwa wakati kama ambavyo makubaliano ya mkataba yanataka, tusiwakatishe tamaa Wazabuni kwani wanashindwa kuomba kazi kwenye taasisi nyingine kwa kucheleweshwa malipo.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Doroth Kobelo amesema
Changamoto za Mfumo sasa zinaenda kupatiwa ufumbuzi na ule ucheleweshaji wa wazabuni kulipwa au kununua vifaa hautakuwepo, tutafuata maadili na kuahidi kutumia mfumo katika manunuzi yote ya Umma.
Mafunzo yametolewa na Wataalamu wa Manunuzi kutoka PPRA Kanda ya Nyanda Za Juu Kusini akiwamo ndugu Anthony Masau, Daniel Kimaro na Ndugu Eliasi Butimbi.
Mafunzo ya Matumizi ya Mfumo wa NeST yanaendeshwa na PPRA kwa muda wa siku 2 kwa watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga , Walimu Wakuu, Walimu wa Manunuzi Shuleni, Wakuu wa idara na vitengo na Maafisa Bajeti na manunuzi wa kila Idara na yamefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari JJ Mungai Mafinga.
NeST ni Mfumo Mpya wa Kielekroniki wa Manunuzi ya Umma. Mfumo wa NeST umeanzishwa ili kurahisisha michakato wa manunuzi na ununuzi wa Umma kuwa wazi, viwango na rahisi.
Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga wakifatilia kwa ukaribu mafunzo ya kujengewa uwezo ya mfumo wa manunuzi Nest ambayo yameendeshwa na PPRA nyanda za juu kusini.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.