RC- SERUKAMBA KUMALIZA KIZUNGUMKUTI CHA VIBANDA 331 VYA BIASHARA KATIKA SOKO LA MAFINGA.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Peter Serukamba leo tarehe 5/4/2024 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Iringa amezungumza ma Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga na kuahidi kumaliza kizungumkuti cha Vibanda331 vya Biashara katika Soko la Mafinga na kuahidi kukutana na mmiliki wa kila kibanda kabla ya mwezi wa tano.
“ Kama kuna Mheshimiwa Diwani au Mtumishi anachochea kutomalizika kwa maridhiano ya vibanda hivi ajiandae. Nitahakikisha mimi na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa tunakuja kuweka Kambi na kukutana na Mmiliki wa kila kibanda, nasisitiza sio mpangaji Mmiliki wa kibanda na hapo taratibu nyingine zitafuata.”
“Aidha kuhusu mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana wanawake na watu wenye ulemavu, Kama kuna mtumishi au Mheshimiwa Diwani anajua alichukua fedha hizo za vikundi ahakikishe ndani ya mwezi mmoja amerudisha fedha hizo, sina utani katika hili”
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa amesisitiza mambo yafuatayo:-
Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani,
Ukamilishaji wa Miradi ya Maendeleo
Afua za Lishe
Taarifa ya M-mama
Taarifa ya CAG.
Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuhakikisha Miradi ya Maendeleo inasimamiwa ili ikamilike kwa wakati na Juhudi ziongezwe katika ku kusanya mapato ya Serikali kwani mapato yakikusanywa na Maendwleo yanapatikana.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa George Kavenuke, KATIBU Tawala Mkoa wa Iringa Bi, Dorise Kalasa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt . Linda Salekwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Fidelica Mnyovella.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.