Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt.Linda Salekwa amewahakikishia kuendelea kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wafanyabiashara na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na amewashauri wawekezaji inapotokea changamoto hakuna haja ya kusubiri vikao badala yake wafike ofisi husika za Serikali na changamoto zitatatuliwa kwa manufaa ya Wilaya na Taifa kwa UJUMLA.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua Baraza la Biashara la Wilaya ya Mufindi lililofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Luganga na kuhudhuriwa na wajumbe wa Baraza la Biashara na Wataalamu.
Mheshimiwa Dkt Linda Salekwa amesema Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa Sekta binafsi katika kuchangia pata la Serikali kupitia Kodi, ushuru na Gozo mbalimbali.
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Frank Sichalwe amesema Ni vizuri watendaji wa Serikali kuhakikisha huduma tunazo toa kwa wawekezaji Ziwe za hali ya juu bila mapungufu na zaidi tuhakikishe huduma zote zinatolewa sehemu moja ili kuwapunguzia mzigo wawekezaji na zaidi kuepusha mianya ya rushwa.
Akizungumza Ndugu Boniface Mlinga Katibu wa TCCIA Wilaya ya Mufindi amesema Hakika ushirikiano wanaoupata wawekezaji kutoka kwa Watendaji wa Serikali kutoka TFS, TRA na Halmashauri za Wilaya za Mufindi ni kubwa. Hivyo tuhakikishe Elimu inazidi kutolewa kwa wawekezaji na wafanyabiasha
Katika Baraza hilo la biashara taarifa kutoka Tanesco, TRA, TFS na Halmashauri za Wilaya ya Mufindi ziliwasilishwa kwa wajumbe kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi hizo na utekelezaji wa majukumu yao.
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga Tc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.