HALMASHAURI YA MJI MAFINGA YAKABIDHI MADARASA 10 YA KIDATO CHA KWANZA -2023 KWA MKUU WA MKOA WA IRINGA.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Saad Mtambule kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amepokea madarasa kumi kutoka kwa Halmashauri ya Mji Mafinga yaliyokamilika yenye thamani ya shilingi milioni 200 fedha kutoka Serikali Kuu kwaajili ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.
Akipokea madarasa hayo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amesema Serikali imejitahidi kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa ili wanafunzi waweze kusoma kwenye mazingira bora ili kuboresha hali ya ufaulu na mazingira mazuri ya kusomea hivyo walimu wahakikishe ufaulu wa Shule na matokeo chanya yaendane na ubora wa majengo.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.