UJENZI WA MADARASA MATATU NA OFISI MOJA SHULE YA SEKONDARI CHANGARAWE (FEDHA ZA TOZO)-MAFINGA TC
Ujenzi wa vyumba vitatu na Ofisi katika Shule ya Sekondari Changarawe ulianza kutekelezwa mwezi Disemba 2019. Ujenzi kuanzia hatua ya Msingi hadi kukamilisha ikiwa ni pamoja na ununuzi wa samani umeshirikisha Serikali kuu, nguvu za wananchi na Halmashauri.
Lengo la Mradi huu ni kufanikisha adhma ya Serikali ya Kuboresha Mazingira ya kufundishia na kujifunzia na hatimae kupata ufaulu mzuri kwa wanafuzi ambao watakuwa watalamu wa Nyanja mbalimbali kwa kuajiriwa ama kwa kujiajiri wenyewe.
Mradi huu wa Ujenzi wa Vyumba vitatu vya madarasa Changarawe Sekondari umegharimu kiasi cha Sh. 59,732,915.00 kati ya fedha hizo wananchi walichangia shilingi 1,800,000.00, Halmashauri shilingi 19,432,915.00, Mfuko wa jimbo Sh 1,000,000.00 Serikali Kuu kupitia fedha za TOZO ya miamala ya simu shilingi 37,500,000.00
Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Happiness Laizer amesema wananchi wa Kata ya Changarawe walionyesha juhudi kubwa kwa kuanzisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja mwaka 2019 kwa kuona na kuthamani mchango wa Wananchi Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani ikachangia kiasi cha shilingi milioni 19,432,915.00 na baadae Serikali Kuu ikalete kiasi cha shilingi milioni 37,500,000.00 fedha ya TOZO ya miamala ya Simu ili kukamilisha madarasa hayo ambayo yamekamilika.
Wananchi wa Halmashauri ya Mji Mafinga wanatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi thabiti wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada mbalimbali za kuleta Maendeleo Halmashauri ya Mji Mafinga.
Wanufaika wa mradi huu ni jamii ya Kata ya Changarawe na maeneo ya jirani.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO-MAFINGATC
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.