Afisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga Ndugu Stephen Shemdoe amehudhuria Mahafali ya kwanza ya kuhitimu Kidato Cha Nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamalala katika Mji wa Mafinga kwenye Viwanja vya Shule hiyo na Kuwatunuku Vyeti Wahitimu hao na kuwasisitiza Wazazi kuzingatia Malezi ya Wanafunzi.
Akiongea katika Mahafali hayo Ndugu Shemdoe amesema Wazazi ni Wajibu wao kuwalea Wanafunzi vizuri kwa kufuata Misingi ya Nidhamu pia Wanafunzi walelewe kwa kufundishwa Maadili kwa kuepuka Ngono,Uvutaji bangi na vitendo hatarishi vinavyohusisha uvunjivu wa Amani pia Wanafunzi wafundishwe Kazi za mikono kama kulima bustani za Mboga na Matunda ambazo zinaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi bila kutegemea Wazazi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Nyamalala Ndugu Jimu Nziku amesema anashukuru Uongozi wa Shule kwa kuonyesha Ushirikiano na Wazazi wa Wanafunzi pia amewasihi Wanafunzi waliohitimu Kidato Cha Nne Kuzingatia mafundisho waliyofundishwa Darasani wanapokwenda Kufanya Mitihani pia wawe Kioo kwa Jamii wanayokwenda kuishi nayo.

"Zingatieni Nidhamu na Maadili Mliyofundishwa na Wazazi na Walimu wenu kwa kipindi Cha Miaka minne Mliyotumia kusoma na Mkawe mfano Bora wa kuigwa kwa Jamii" amesisitiza Ndugu Nziku.
Naye Mzazi wa Wanafunzi waliohitimu Kidato Cha Nne Bi;Ajentina Kilufi amesema kwa niaba ya Wazazi anashukuru Mungu kwa Wanafunzi Kuhitimu pia anashukuru Wazazi na Walimu kwa Malezi na Elimu waliyowapatia Wahitimu hao na Jitihada za Mkuu wa Shule katika Usimamizi wa Walimu, Wanafunzi na Miradi ya Maendeleo ya Shule.

Pamoja na hayo Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyamalala Ndugu Ezekieli Mwakalomba amesema anawapongeza Wahitimu wote wa Kidato Cha Nne kwa kuzingatia Malezi, Nidhamu na Elimu waliyopewa hapo Shuleni hivyo wakawe Vioo kwa Jamii,pia amemshukuru Mhe;Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia Fedha za Ujenzi na Uongozi wa Halmashauri ya Mji Mafinga ukiongozwa na Mkurugenzi Bi; Fidelica Myovella na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari kwa kuwasimamia kikamilifu katika Mipango ya Maendeleo ya Ujenzi wa Shule.
Nasri Mwinyi
Afisa Habari- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.