Wilaya ya Mufindi imeendesha Baraza la Wafanyabiashara ampambo wamejadili mambo mbalimbali ili kuhakikisha Wilaya na Halmashauri zake zinakusanya mapato.
Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya Mufindi Afisa Tawala Ndugu Robert Kilewo ambaye ameongoza Baraza hilo amewasisitiza wafanyabishara na waekezaji kuhakikisha wanalipa kodi stahiki za Serikali na kuhakikisha wanatumia mashine za kieletroniki kutolea risiti.
Aidha kwa upende wa Wawekezaji wa viwanda vya mazao ya misitu amewataka kuhakikisha wanatumia mizani katika kupima magogo ili kuweka usawa katika biashara hii na kuacha kukadiria jambo linalopelekea kupata hasara kwa wauzaji wa magogo katika viwanda hivyo.
Pia amewataka wafanyabiashara wa magogo kuunda umoja wao na kuwa na katiba na uwongozi ambao utawasaidia na kufatilia mambo ambayo tumekubaliana na wawekezaji wa viwanda vya mazao ya misitu na kutatua kero mbalimbali ambazo wamekuwa wakizipata katika biashara hii ya magogo.
Hata hivyo ametoa rai kwa Maafisa Biashara wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kuhakikisha wanaandaa maonyesho ya biashara ya Wilaya ya Mufindi ili kuweza kutangaza biashara zetu na malighafi zetu ili tuweze kuwavutia wawekezaji katika Wilaya yetu na kukuza uchumi na pato la mtu moja moja.
Aidha amezitaka Sekta binafsi kuendelea kushirikiana na Serikali kwakuendelea kuzalisha na kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa viwanda vya misitu, na kuongeza samani katika bidhaa zao ili kuweza kukuza soko la bidhaa za ndani na kukuza uchumi na pia kuhakikisha bidhaa zinazo zalishwa kutoka Wilaya ya Mufindi zinaweza kutambulika sehemu ambayo imetengenezwa.
Michael Ngowi
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.