Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer(Sasa Mkurugenzi Monduli)amemkabidhi ofisi Mkurugenzi wa Sasa Ndugu, Ayoub Kambi.
Akikabidhi sheria, miongozo na kanuni za Halmashauri Bi, Happiness Laizer amesema kuwa Lengo la Mheshimiwa Rais ni kuona wananchi wanapewa huduma bora, miradi ya maendeleo inasimamia kwa ufanisi na mapato yanakusanywa hivyo uwepo wako hapa mafinga umeaminiwa na Mheshimiwa Rais na ushirikiano wa watumishi utakusaidia katika utendaji wako wa kazi.
Aidha amewaomba watumishi na wakuu wa Idara kumpa ushirikiano Mkurugenzi Ayoub Kambi ili kazi yake iwe rshisi na afikie malengo.
Naye Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu, Ayoub Kambi amesema ataendelea pale alipoishia Bi, Happiness na kuomba ushirikiano na wakuu wa Idara ili kuweza kufikia malengo ya Mheshimiwa Rais ya kutatua kero na shida za wananchi
Akihitimisha Hafla hiyo ya makabidhiano, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema hakika Mkurugenzi Lazer aliweza kufikia malengo kwenye sekta ya elimu Mafinga iliongoza, mapato iliongoza kwa mwaka 2021/2022 na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
“Mkifanya vizuri nyie wataalamu kwenye kukusanya mapato, kusimamia Miradi ya Maendeleo sisi waheshimiwa Madiwani tunatembea kifua mbele, tukuhakikishie Mkurugenzi Ayoub Kambi ushirikiano kutoka kwa waheshimiwa madiwani na wataalamu ili uweze kufikia malengo yako.Pia tukutakie kila lakheri Mkurugenzi Bi, Happiness Laizer kwenye kituo chako kipya cha kazi na tukupongeze kwa kuendelea kuaminiwa na Rais.
Tarehe 7 Juni, Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alifanya Teuzi za Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya ambapo katika Uteuzi huo Ndugu Ayoub Kambi aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mji Mafinga na Bi, Hqppiness Laizer kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Makabidhiano yamefanyika katika Ukumbi wa Mkurugenzi na kuhudhuriwa na waheshimiwa Madiwani wa Kamati ya Fedha na wakuu wa Idara Halmashauri ya Mafinga.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.