ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MHE. SAAD MTAMBULE(sasa DC Kinondoni) AKABIDHI RASMI OFISI KWA MKUU WA WILAYA YA MUFINDI MHE. DKT. LINDA SALEKWA- MAFINGA
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amemkabidhi rasmi Ofisi Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya na Kumkabidhi taarifa ya Wilaya na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi.
Amesema Wilaya ya Mufindi ipo Salama kwa watu kuishi na wawekezaji kuwekeza kwa viwanda, kilimo na biashara mbalimbali kwani huduma zote muhimu za kijamii zinapatikana.
Mheshimiwa Mtambule ameongeza kuwa anawashukuru sana viongozi na wananchi wa Wilaya ya Mufindi kwa ushirikiano Mkubwa waliomuonyesha na kuhakikisha Miradi ya Maendeleo inasimamiwa na inatekelezwa kwa wakati.
Ameomba Ushirikiano Mkubwa uendelee kwa Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa ili kumrahisishia utendaji wake wa Kazi.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ofisi. Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amesema anamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na ameahidi kumuwakilisha vyema katika Wilaya ya Mufindi na kushirikiana na wananchi katika Utekekezaji wa Miradi ya Maendeleo na shughuli zote za Kiuchumi na Kijamii.
“ Naomba Ushirikiano wenu viingozi, wananchi na wataalamu nipo tayari kufanya kazi Mufindi na ninawaahidi ushirikiano wa kutosha, lengo ni kuiinua Mufindi na nitaanzia pale ambapo Mtangulizi wangu Mheshimiwa Saad Mtambule ameachia”
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-
Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.