• Malalamiko |
    • Wasiliana na sisi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
Mafinga Town Council
Mafinga Town Council

Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mafinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Kilimo na umwagiliaji
      • Fedha
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya
      • Ardhi na Maliasili
      • Community Development,Social welfare Gender and Youth
      • Water
      • Work
    • Vitengo
      • Community
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Huduma za Kisheria
      • Biashara
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa madiwani
    • Kamati Za Kudumu Za Halmashauri
      • Fedha Na uongozi
      • Mipangomiji Namazingira
      • Uchumi, Fedha Na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana Na Mwenyekiti
  • Miradi Mbalimbali
    • Progressive projects
    • Itakayo Tekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Machapisho ya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Makitaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Malalamiko

Ally Hapi atamani Rais Magufuli aweke jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya utawala ya halmashauri ya mji mafinga.

Posted on: September 17th, 2018

Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Ally Salum Hapi ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya “Iringa Mpya” ya tarafa kwa tarafa alipotembelea, kukagua na kuridhika na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi za utawala zinazojengwa kwa pesa za serikali chini ya kampuni ya ujenzi ya SUMAJKT katika eneo la luganga mjini mafinga wilayani mufindi mkoani iringa.

Amewataka wakala wa majengo ya serikali (TBA) kusimamia mradi huo ipasavyo ili viwango vilivyoanishwa vionekane na thamani ya fedha iliyotumika nayo ionekane na kama Mhe Rais akija Mafinga basi Mkuu wa Mkoa Iringa anatamani Mhe Rais aweke jiwe la msingi la jengo hilo ili aone fedha anazotoa za serikali zinafanya kazi.

“Hivyo kwa kipekee nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe DKT. John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuleta fedha hizi kwa ajili ya kujenga jengo hili kwa wananchi wa Mafinga na ni imani yangu kwamba watu wengi zaidi ya 200 hapa wamepata ajira kwa hiyo sehemu kubwa ya fedha imerudi mifukoni mwa wananchi na akina mama wapo hapa wanauza chakula kwa mafundi” alisema Mhe Hapi.

Aidha ametoa rai kwa wasimamizi na waliopewa dhamana ya kusimamia miradi wahakikishe wanaisimamia vizuri ili fedha ya serikali itumike kwa makusudi na dhamira iliyokusudiwa.

“Mradi huu na miradi mingine yote, Wakurugenzi mnawajibika kuisimamia ipasavyo na kufuatilia kwa makini ili kuhakikisha kila senti ya serikali inayoletwa hapa inatumika kwa makusudi yaliyopangwa” alisema Mhe Hapi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Saada Mwaruka aliishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia fedha na kuanza kwa ujenzi huo unaotarajia kukamilika tarehe 30 Machi , 2019.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi huu ambao hadi kukamilika utaondoa adha tuliyonayo kwa sasa ya uhaba wa vyumba vya ofisi na ukumbi wa mikutano” alisema Bi Saada Mwaruka.

Changamoto ya uhaba wa ofisi za idara na vitengo iliyopo sasa ilipelekea kuwasilisha ombi serikali kuu kuwezeshwa fedha za ujenzi wa jengo la utawala.

Na katikati ya mwaka 2016/2017 iliidhinishiwa bajeti ya ujenzi wa jengo la utawala.

Ujenzi wa jengo hilo unagharimu jumla ya kiasi cha zaidi ya tshs bilioni 3.38 mpaka kukamilika, lakini mpaka sasa Halmashauri imepokea jumla ya tshs bilioni 2 kwa awamu mbili tofauti awamu ya kwanza mwaka wa fedha 2016/2017 ilipokea jumla ya tshs. milioni 500 na awamu ya pili mwaka wa fedha 2017/2018 ilipokea jumla ya tshs. bilioni 1.5

Fedha hizo ni kutoka wizara ya fedha na mipango kupitia ruzuku ya miradi ya maendeleo mpaka sasa jumla ya tshs. Bilioni 1.3 zimetumika.

Mradi huo unajengwa na mkandarsi National Services Construction Department (SUMAJKT) kwa gharama ya tshs bilioni 3.38 chini ya mkataba namba LGA.169/2016-2017/HQ/W/06 na unasimamiwa na wakala wa majengo wa serikali (TBA).

Ujenzi ulianza kwa kupima udongo na kufuatiwa na kazi ya kuchimba msingi wa jengo, kumimina nguzo na linta zake, kumimina sakafu hadi ghorofa ya kwanza. Mpaka sasa ujenzi huu umefikia asilimia 60 ya mpango kazi (Framework).

Kazi zinazoendelea kufanyika kwa sasa ni kupiga lipu ghorofa ya chini na kujenga kuta ghorofa ya kwanza.

Aidha, kwa kuzingatia mpango kazi wa mkataba mkandarasi yupo mbele ya ratiba kwa mwezi mmoja.

Hadi kukamilika kwa mradi huu utawezesha Halmashauri ya Mji kuwa na ofisi za uhakika kwa ajili ya utoaji wa huduma na kuondoa adha ya uhaba wa vyumba vya ofisi.

Wakati wa utekelezaji wa mradi huo umekuwa na manufaa kwa wakazi wa Mji wa Mafinga na maeneo yanayozunguka eneo la mradi kwani umekuwa ni chanzo cha kipato kwa kupitia ajira za muda mfupi na wafanyabiashara wadogo wadogo na wakubwa.

Jumla ya wakazi 211 kati yao wanawake 68 na wanaume 143 wamepata ajira kutokana na mradi huu.

Mradi wa ujenzi wa jengo la utawala katika Halmashauri ya Mji Mafinga ulianza kujengwa tarehe 22.9.2017 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 machi 2019.

Halmashauri ya Mji Mafinga ilianzishwa tarehe 01, Julai 2015, ikianzishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Wakati inanzishwa ilikuwa na uhaba wa ofisi za kuwezesha idara na vitengo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, Halmashauri ililazimika kuazima baadhi ya majengo ya Halmashauri ya Mufindi na kuyatumia kama Ofisi ya Halmashauri ya Mji Mafinga.

Matangazo

  • NAFASI ZA MASOMO KWA SHULE YA CHIEF MKWAWA ENGLISH MEDIUM- HALMASHAURI YA MJI MAFINGA. NAFASI BADO ZIPO TUPIGIE January 29, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YANAPATIKANA www.mafingatc.go.tz July 13, 2024
  • MJI MAFINGA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI MAPATO YAKUSANYA ASILIMIA 113 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024 August 14, 2024
  • MATOKEO YA DARASAM LA SABA 2024 YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI YETU .www.mafingatc.go.tz October 30, 2024
  • View All

Habari mpya

  • VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VIFUNGWE MFUMO WA GoT-HOMIS

    June 20, 2025
  • HALMASHAURI YA MJI MAFINGA YAPATA HATI SAFI YA UKAGUZI KUTOKANA NA TAARIFA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KWA HESABU ZINAZOISHIA TAREHE 30 JUNI 2024

    June 19, 2025
  • HALMASHAURI YA NKASI YAITEMBELEA MAFINGA MJI KUBADILISHANA UZOEFU

    June 18, 2025
  • MWANZA NA DODOMA ZATINGA FAINALI SOKA WAVULANA UMITASHUMTA 2025

    June 17, 2025
  • View All

Video

SENSA NI MAENDELEO
Video zaidi

Viungo Vya Haraka

  • Maelezo na Form Ya kiapo cha uadilifu
  • https://matokeo.necta.go.tz
  • Muongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya wananchi

Watembeleaji kidunia

world map hits counter

Idadi ya watu wanao tembelea Tovuti

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana na sisi

    Mafinga Town.

    Postal Address: Po.Box 76 Mafinga

    Simu: +255 262 772 393

    Mobile: 026-2772393

    Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.