Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe, Regnant Kivinge amepongeza Kamati zote kwa Kasi nzuri iliyofanyika kwa Kipindi chote cha Robo ya pili amemshukuru Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella na timu yote ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Mji Mafinga kwa namna ambavyo wamekuwa wakifanya kazi kwa kujitoa na pia amewapongeza kwa hatua ya haraka waliyochukua katika kuthibiti sitofahamu ya masuala ya misaada ya dawa pia alichukua nafasi iyo kuwaambia Watumishi wawatoe watu hofu kwani Serikali imesikia na lazima itachukua hatua za haraka.
Aidha Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi (DAS) Ruben Chongolo amewakumbusha wataalamu wa Mji Mafinga mambo mbalimbali ya kuzingatia ikiwemo utoaji wa vibali vya ujenzi ambavyo amewataka kufuata utaratibu wa mipango miji. Pia amechukua nafasi hiyo kuwapongeza idara ya ukusanyaji mapato “Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya ata mimi binafsi nimeshuhudia usiku mkikusanya mapato” amesema DAS Ruben Chongolo.
Baraza ilo la Madiwani ambalo limehudhuliwa na Katibu Tawala, Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi wa Mji Mafinga, Wataalamu wa Mji Mafinga pamoja na Wananchi.
Na,
Anna Mdehwa,
Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.