Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Mji Mafinga limepitia Rasimu ya Mpango wa Bajeti wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa mwaka wa Fedha 2025/2025. Akifungua kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella amewataka wajumbe kuwa huru kutoa mawazo yao sehemu ambayo wanatamani ifanyiwe maboresho au kutoa ushauri lengo likiwa ni kahakikisha vipaumbele vya Halmashauri vinaguswa katika Bajeti ya 2025/2026
Akiwasilisha rasimu hiyo ya Bajeti ya 2025/2026 kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Mji Mafinga Afisa Mipango Mji Mafinga Ndugu Peter Ngussa amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri inakadiria kutumia Jumla ya Tsh. 31,458,031,000.00 kati ya fedha hizo Tsh. 7,538,590,000.00 zitatokana na mapato ya ndani, Tsh. 942,454,000.00 ni ruzuku ya matumizi mengineyo (OC), Tsh. 17,395,844,000.00ni ruzuku ya mishahara na TZS 5,581,143,000 ni ruzuku ya Miradi ya Maendeleo.
Ngusa amesema Halmashauri katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 imejiwekea vipaumbele vinne ambavyo ni:-
-Kutekeleza miradi inayolenga kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani (Own Source), mathalani:
Kununua maeneo ya uwekezaji,
Kuendeleza ujenzi wa miradi ya kimkakati,
Kuendeleza shamba la parachichi Makalala,
Kutunga na/au kuhuisha sheria ndogondogo za ukusanyaji wa mapato.
-Kuboresha utoaji wa huduma za jamii kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii kwa ukamilisha/kujenga miundombinu ya Sekta
-Kuboresha ustawi wa wananchi kwa kuimarisha utawala bora kwa kuzingatia: demokrasia, utawala wa Sheria, haki, ushirikishwaji wa wananchi.
-Kuimarisha Hali ya usafi na Uhifadhi wa Mazingira katika Mji wa Mafinga.
Aidha wajumbe wa Baraza walishauri kuhusu namna ya kuwapata wafanyakazi bora -Mei Mosi, Nyumba za wafanyakazi na madeni ya wafanyakazi ambapo Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovellal alitolea ufafanuzi kuwa bajeti hii ya 2025/2026 imezingatia masuala yote na ushauri wote uliokuwa umitolewa kwenye vikao vya wafanyakazi umefanyiwa kazi.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.