BENKI YA CRDB- MAFINGA katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja imetembelea Ofisi Kuu Halmashauri ya Mji Mafinga kukutana na Timu ya Menejimenti ikiongozwa na Mkurugenzi Ndugu, Ayoub Kambi ikiwa ni kutambua mchango wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Benki ya CRDB na kufafanua fursa mbalimbali zinazopatikana CRDB BENKI.
Akizungumza Meneja CRDB Kanda ya Kati Bi, Chabu Mishwaro amesema kila wiki ya Kwanza ya mwezi wa kumi Ni Wiki ya Huduma kwa Wateja hivyo, CRDB inatambua na kuthamini mchango wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa ustawi wa Benki ya CRDB kwani MJI MAFINGA ni Taasisi mteja katika Benki hiyo.
“ Lengo la CRDB ni kusogeza Taasisi hii Karibu kabisa na wananchi na kuhakikisha CRDB Inasonga mbele.
Tuna fursa nyingi sana kwenye Benki yetu ya CRDB ikiwemo Uwekezaji- Akaunti Maalumu, Dhahabu, Green bond, IMBEJU,Bima, wastaafu, TAUSI. Fursa hizi zote zinatolewa na Benki ya CRDB. Hivyo tupo hapa kwanza kuthamini mchango wenu na Pia kuwapa fursa hizi kutoka Benki ya CRDB”
Amesema CRDB Ipo tayari kuendelea kufanya kazi na Halmashauri ya Mji Mafinga Hasa katika Sekta ya Uwezeshwaji Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi kwa kuendelea kuyainua makundi hayo kutoka katika Umaskini na kuwainua kiuchumi.
Nae Meneja wa CRDB Tawi la Mafinga Ndugu Lusekelo Haidi amesema uongozi wa Mji Mafinga umekuwa ukiwapa ushirikiano wa Kutosha benki ya CRDB na Akaunti zimekuwa zikifunguliwa kutoka Wadau mbalimbali wa Halmashauri.
Akitoa Shukrani Kwa niaba ya Timu ya Menejimenti Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu Ayoub Kambi amesema hakika Benki ya CRDB Ina fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuisaidia Halmashauri hivyo akawaomba Wakuu wa Divisheni za Mipango, Biashara na Fedha Kukaa na watalaamu kutoka CRDB na kuona jinsi ambacho wanaweza kuisaidia Halmashauri kwenye Masuala mbalimbali yahusuyo uwekezaji na Miradi ya Maendeleo.
Mada mbalimbali zimewasilishwa na watalaamu kutoka CRDB KANDA YA KATI na baadae wamempongeza Mkurugenzi wa Mji Mafinga kwa Kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano- Serikalini -MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.