Benki ya Dunia na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Mafinga wameendesha kikao cha wataamu kujadili maandalizi ya mpango wa utekelezaji wa miradi ya TACTIC awamu ya tatu katika Halmashauri ya Mji Mafinga.
Katika kikao hicho ambacho kimeshirikisha wadau mbalimbali ambao wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza na kutoa ushauri na maelekezo ili kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kama ambavyo imepangwa.
Aidha kikao hicho kimeweza kupitia na kuona michoro mbalimbali ya miradi ambayo inatakiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Mji Mafinga kutoka kwa Muandisi Mshauri Kampuni ya BOTEC.
Pia wataalamu hao wamepitia na kungalia maeneo ambayo yatatumika kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa Barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 11.83 ujenzi wa Stendi ya kisasa eneo la Kinyanambo na ujenzi wa soko la kisasa na kutoa maelekezo mbalimbali ikiwemo ushirikishwaji wa jamii ili kuelewa umuhimu wa miradi hii katika maeneo yetu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Fedelica Myovella amesema kuwa ameshukuru ujio wa taalamu hao kwa kuja kuwajengea uwelewa timu ya wataalamu wa Halmashauri ambao wanasimamia miradi ya TACTIC na pia kufanyia kazi malekezo na mapendekezo yaliyotelewa na wataalamu hao mapema ili kuhakikisha miradi hiyo inaanza kutekelezwa katika Halmashauri yetu .
Michael Ngowi Afisa Habari.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.