BENKI YA NMB MAFINGA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA KWA KUKABIDHI VITANDA 8 VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 5 KWA ZAHANATI YA RUNGEMBA - MAFINGA MJI.
Akizungumza Meneja wa NMB Tawi la Mafinga Bwana Focus Simeon Lubende akiwa ameambatana na Beatrice Kalutu Meneja kutoka NMB Makao Makuu amesema NMB katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja inaungana na Serikali katika kuhakikisha inatokomeza vifo vya Mama na mtoto kwa kukabidhi vitanda 4 vya wakina mama kujifungulia na vitanda 4 kwa wagonjwa wa kawaida vyenye thamani ya shilingi milioni ppp.

Amesema NMB inautaratibu wa kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii hasa katika sekta ya Elimu na Afya, hivyo kutokana na Mahusiano Mazuri ya Serikali na NMB Focus imeahidi kupitia NMB kuendelea kutoa sehemu ya faida kwa jamii na kushirikiana na Serikali katika nyanja zote hususan Elimu na Afya na kuomba wananchi kuendelea kuitumia NMB.
Akishukuru kwa Msaada huo Mkurugenzi Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa ameishukuru Benki ya NMB tawi la Mafinga kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuchangia Maendeleo ya Nchi hasa katika kuzuia vifo vya Mama na Mtoto.

Amesema vifaa hivyo vitatunzwa ili viweze kutoa huduma kwa jamii kama ambavyo lengo la NMB lilivyo katika kuchangia faida yake kwa Jamii hasa katika Sekta ya Elimu na Afya.
Naye mwananchi Bi Atu Kadege ambaye ni Mjumbe wa Ujenzi Zahanati ya Rungemba amesema wanaishukuru NMB kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za Afya na Elimu Tanzania hasa kwa Halmashauri ya Mji Mafinga hususan katika Zahanati ya Rungemba kwa kuipatia vitanda 8 ambapo vitanda 4 vya wakinamama kwaajili ya huduma ya kujifungu na vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida.

Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Mji Mafinga na watumishi mbalimbali wamehudhuria makabidhiano hayo ya NMB katika kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Mteja.
Imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.