Benki ya NMB Tawi la Mafinga imetoa mikopo ya Bajaji 9 , BodaBoda 5 na Guta 1 kwa Wanachama wa Umoja wa Wasafirishaji Mafinga,Hii ni mikopo ya awamu ya pili kutolewa na Benki ya NMB kwa Madereva na Wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.
Akizungumza Meneja wa Benki NMB Tawi la Mafinga, Bw Focus Lubende amezitaja sifa za kuweza kukopa kuwa ni uwe Mwanachama Chama cha Bodaboda au Bajaji,Kuwa mteja wa NMB na kuwa waaminifu katika mikopo wanayopatiwa.
Nae Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Mufindi, Bw Dickson Mtevele ame shauri Jeshi la Polisi lisiwe chanzo cha kuwabambikiza makosa madereva Bajaji na Bodaboda kwa maslahi yao binafsi katika Hafla ya kupokea mikopo ya Bajaji na BodaBoda.Pia ameishauri NMB kuendelea kuwakopesha vijana baada ya miezi mitatu kama wameweza kuwakopesha Bodaboda na Bajaji.
Aidha Mwenyekiti wa Bajaji Bw Harun Manga ameishukuru Benki ya NMB kuwapatia Mikopo ambayo itaenda kuboresha maisha yao.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu wa CCM Wilaya Bi Frida Kaaya,Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mafinga,Afisa Biashara Mafinga Mji Bw Evance Mtikile ,Diwani Kata ya Boma Mheshimiwa Julius Kisoma , Taasisi ya Fedha MUCOBA PLC na Wanachama Wamiliki Bajaji na Bodaboda.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
Christopher Mhina
Mwandishi wa Habari Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.