BILIONI 1 KUTUMIKA KUWEKA TAA 180 ZA BARABARANI KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
Halmashauri ya Mji Mafinga tarehe 5/4/2023 imesaini mkataba na REA wa Shilingi milioni 500 kwaajili ya uwekaji taa 180 za barabarani ambapo Halmashauri ya Mji Mafinga pia itachangia shilingi Milioni 500 na kufanya thamani ya Mradi kuwa Bilioni 1.
Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema Mradi utasaidia Kuongeza na kukuza UCHUMI wa Mji Mafinga na wafanyabiashara kufanya biashara kwa uhuru na usalama wa wananchi wa Mji Mafinga utaongezeka ikiwa ni pamoja na kuweka Muonekano mzuri wa Mji.
“ Mradi huu una thamani ya shilingi Bilioni 1 na unatekelezwa na Pande zote mbili REA na Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo Milioni 500 zitachangiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga kutoka Mapato yake ya ndani na Milioni 500 Ni ufadhili kutoka REA(Wakala wa Nishati Vijijini) “ Kivinge, Mwenyekiti wa Mji Mafinga.
Nae Mbunge wa Mafinga Mjini Mheshimiwa Cosato Chumi amesema ni fahari sana kwa wananchi wa Mji Mafinga kupata Mradi huu wa taa za barabarani ambazo zitawekwa umbali wa kilomita 5.
“ wananchi wa Mafinga wamekuwa wakisubiri Mradi huu kwa shauku sana na wafanyabiashara wa Mji Mafinga watafanya biashara zao Masaa 24, tumepambana sana kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mji Mafinga mpaka mradi umekuja, sasa hizi ni taa kwaajili ya Mji wetu na ni wajibu wetu kuzitunza .
Akitoa takwimu za Mradi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema kuwa Mradi utatekelezwa kwa siku 120 baada ya kusainiwa mkataba na maeneo yatakayoguswa na mradi uwekaji wa taa za barabarani ni
-Kinyanambo A,B,C umbali wa km 1.9
-Mafinga Hospitali km 0.2
-CF plazer- tanki la maji pipeline km 0.4
-NSSF- Bomani km 0.9
-Luganga- Mgololo km 0.1
-Mashujaa - Royal Park Hotel km 0.2
-Chaibora- Dembe km 0.1
-NMB-mashujaa-Mashine ya mpunga km 1.2
Aidha Bi, Laizer ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa malengo yake kupitia Wakala wa Nishati Vijijni REA kuhakikisha wananchi wote Tanzania Hasa maeneo ya vijijini wanapata nishati bora na Mji wa Mafinga unakuwa kiuchumi kwa kuweka taa 180 za barabarani.
Uwekaji saini umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer, Wakili wa Serikali, Msomi Gasper Kalinga, Mwanasheria wa REA Musa Muze na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge, Mbunge wa Mafinga Mjini Mheshimiwa Cosato Chumi na Mkurugenzi wa Uendelezaji masoko na Teknolojia Mhadisi Advera Mwijage Jijini Dodoma.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mafinga Tc
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.