Tuhakikikishe Elimu tunayotoa kwa wananchi kuhusu kilimo cha mboga mboga katika kupambana na Utapiamlo katika Jamii zetu kinakuwa kilimo cha mboga Endelevu kama vile tembele,chainizi,Kisamvu
Akizungumza katika Kikao cha Tathmini ya viashiria vya Mkataba wa Lishe
Kwa Kipindi cha robo ya kwanza 2024-2025 kilichofanyika katika ukumbi wa HAlmashauri ya Mji Mafinga Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Reuben Chongolo amesema, suala la utoaji wa Elimu ya Utapiamlo liwe ni agenda ya kudumu kwenye vikao mbalimbali katika ngazi ya kijiji, Mtaa hadi Kata ili kuwapa ufahamu wananchi ni mboga gani zinafaa katika kapamana na Utapiamlo kwenyr Jamii .
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mikataba ya Lishe Bi Josephine Kazungu Afisa Lishe Halmashauri ya Mji Mafinga amesema kuwa Kwa robo ya kwanza Kata zote 9 zimefanya vikao vyq Maendeleo na Agenda ya lishe ilijadiliwa na hali ya upqtikanaji wa Chakula cha Mchana Mashuleni ambapo ilielezwa kuwa Shule zote zinatoa chakula cha Mchana kwa wanafunzi
Amesema kwa robo ya kwanza Jumla ya wakazi 721 kutoka Kata ya Upendo wamepatiwa Elimu ya Lishe kupitia mikutano ya hadhara katika Mitaa Mitano 5 ya Amani, Balali, Lumwago, Mgodi na Mbagala.
Katika Kikao hicho kilichohudhuriwa na Mkurugenzi Mji Mafinga Bi Fidelica Myovella, Watendaji wa Kata zote 9, Wakuu wa Idara na Vitengo na Maafisa Tarafa kutoka Wilaya ya Mufindi
imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo - Mafinga
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.