Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt linda Salekwa amekabidhi Jumla ya Pikipiki 16 kwa Maafisa Ugani na Kilimo wa Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo pikipiki hizo zitakwenda kutatua kero na changamoto za Wakulima katika kupata taarifa za mbolea .
Akizungumza baada ya kukabidhi pikipiki hizo kwa Maafisa Ugani na Kilimo Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amesema yuko nao pamoja Maafisa Ugani na Kilimo kuhakikisha wanafanya kazi ipasavyo kwani lengo lililokusudiwa ni kufanya kazi kwa vitendo na likawe deni kwao katika kutekeleza shughuli za Mh.Raisi katika kuleta maendeleo pia amesisitiza suala la uwajibikaji kwa kila mtu kwa wakati pasina kusukumwa.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Halmashauri ya Mji Mafinga amesema huu ndio Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lazima wahakikishe wanaisimamia katika katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia amempongeza Mh.Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kuona changamoto zilizokuwepo za vitendea kazi vya Usafiri kwa Maafisa Ugani na Kilimo.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bw. Regnant Kivinge amesema Pikipiki hizo zitakwenda kutatua changamoto za usafiri zilizokuwepo kwa Maafisa Ugani na Kilimo kutoka sehemu moja kwenda nyingine ambazo zilikuwa ngumu kuzifikia ndani ya Halmashauri ya Mji Mafinga,aidha matarajio ya Maafisa Ugani na Kilimo ni kuongeza uzalishaji kwa kiwango cha juu na kuanzisha mashamba darasa kila mahali baada ya kupata pikipiki hizo.
Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi.Happinez laizer,Mkuu wa Idara ya Kilimo Halmashauri ya Mji Mafinga,Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,Maafisa Ugani na Kilimo wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Viongozi wa Ulinzi na Usalama wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
Christopher Mhina
Mwandishi wa Habari Mafinga Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.