Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mhe Saad Mtambule pamoja na uongozi wa halmashauri za mafinga mji na mufindi ameongoza matembezi ya siku ya sherehe za miaka 60 ya uhuru na kusadia wagonjwa na wenye mahitaji maalum.Akiwa katika Hospitali ya Mafinga aligawa sabuni kwa wagonjwa katika wodi mbalimbali.Pia aliongoza harambee ya kumchangia mgonjwa fedha za nauli kiasi cha 145,000/= ili zimuwezeshe mgonjwa huyo(pichani) kufika mkoa wa kagera wilaya ya biharamuro.Mgonjwa huyo jina limehifadhiwa alifika hospitali mafinga kwa matibabu lakini hakuwa na ndugu.Baada ya kutibiwa uongozi wa hospitali uliwatafuta ndugu zake na kupatikana.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.