SHULE MPYA NANE ZA SEKONDARI/MSINGI ZAJENGWA 2021-2025 KATIKA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA
Halmashauri ya Mji Mafinga kwa kipindi cha mwaka2021 hadi 2025 imefanikiwa kujenga shule mpya 8 ikihusisha 5 za sekondari na 3 za msingi lengo likiwani mkakati endelevu katika kukuza maendeleo katikasekta ya elimu.
Akiongea katika ofisi za Halmashauri Mji MafingaMkurugenzi Bi,Fidelica Myovella amesema ‘’shule za sekondari zilizojengwa katika mwaka 2021-2025 niItimbo, Mgodi, Sao Hill, Amali na Ndolezi lakini pia kumeanzishwa shule mpya za Bumilayanga B na shuleya sekondari ya wasichana ya Mafinga ambazozinatarajiwa kusajiliwa mwaka wa fedha 2025/2026.’’
Naye Afisa Elimu Sekondari mwalimu stephen Shemdpoe amesema kuwa kwa miaka minne kupitia mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali kuu Halmashauri imeweza kujenga shule hizo nane lengo likiwa ni kutekeleza malengo ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kwa gharama nafuu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.