Mpaka kufikia Aprili 2025 vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya katika Halmashauri ya Mji Mafinga vimefungwa mfumo wa GoT-HOMIS, hatuna kituo ambacho hakijafungwa mfumo huu”
Kauli hiyo imetolewa na Bi. Matilda Daudi Yassin Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Mafinga alipokuwa akiongea na Mwandishi wa Habari hii katika Ofisi za Halmashauri Lugangq.
Matilda amesema Halmashauri ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 26 na vituo 16 vilikuwa havijafungwa mfumo huu lakini mpaka sasa vituo hivyo 16 navyo vimefungwa Mfumo huu mpaka mwezi wa Nne tumekamilisha.
Amevitaja vituo hivyo 16 kuwa ni Ihongole, Ifingo, Upendo, Changarawe, Saohill, Kikombo, Mtula, Matanana, Ulole, Bumilayinga, Kisada, Isalavanu, Rungemba, Itimbo,Kitelewasi na Hospitali ya Mji Mafinga.
Kaimu Mganga Mkuu amesema Mfumo Unachochea Ongezeko la Ukusanyaji wa Mapato ya Kituo kwani unaongeza mapato sahihi ambayo yanqkusanywa na kituo husika.
GoT-HOMIS ni mfumo wa Kieletroniki ulioanzishwa kwaajili ya Usimamizi na Uendeshaji wa Vituo vya Kutolea huduma za Afya.
Na: Sima Mark Bingileki
Afisa Habari Mkuu
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.