TAA ZA BARABARANI ZA UMEME JUA HATUA MPYA YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MJI MAFINGA.
Halmashauri ya Mji Mafinga imetekeleza Mradi wa Taa za Barabarani za umeme jua ambapo jumla ya Taa 180 zimefungwa kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo kwa awamu ya kwanza Halmashauri ya Mji Mafinga imechangia shilingi Milioni 295,000,000.
“Mradi huu una thamani ya shilingi Bilioni 1 mpaka kukamilika kwake na unatekelezwa na pande zote mbili REA na Halmashauri ya Mji Mafinga kutoka Mapato yake ya ndani itatoa milioni 500 na ufadhili kutoka REA milioni 500 pia amesema kukamilika kwa huu Mradi utakuza shughuli za kiuchumi hasa nyakati za usiku”. Amesema Bi Fidelica Myovella Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga
Bi, Fidelica ameelezea kuwa mpaka kukamilika kwa huu mradi maeneo yatakayokuwa yamewekwa taa za barabarani ni
-Kinyanambo A,B,C km 1.9
-Mafinga Hospitali km 0.2
-CF plazer- tanki la maji pipeline km 0.4
-NSSF- Bomani km 0.9
-Luganga- Mgololo km 0.1
-Mashujaa - Royal Park Hotel km 0.2
-Chaibora- Dembe km 0.1
-NMB-mashujaa-Mashine ya mpunga km 1.2.
Naye Bwana Japheth Sanga Mwananchi wa Halmashauri ya Mji Mafinga ameishukuru Serikali kwa kupitia Halmashauri ya Mji Mafinga kwa taa zilizowekwa kwa awamu ya Kwanza kwani zimerahisisha ufanyaji wa biashara nyakati za usiku
“Kwakweli izi taa zimerahisisha sana ufanyaji wa biashara nyakati za usiku kwani mwanzo tulikuwa tunafunga mapema giza tu likikaribia kuingia lakini sasa ivi tunaweza kaa mpaka saa nne usiku na Mji wetu unapendeza sana” Amesema Japheth Sanga.
Mradi wa Taa za Barabarani za umeme jua kwa awamu ya kwanza zilianza kufungwa mwezi wa Saba 2024 na mpaka kukamilika kwake zimefungwa taa 180.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.