“ Kila mwekezaji mwenye Kiwanda ahakikishe kwenye kiwanda chake kuna akiba ya maji kuanzia lita laki 1 kwaajili ya majanga ya moto pindi yanapotokea kulingana na shughuli zinazofanywa kiwandani hapo au eneo la jirani.”
Kauli hiyo imetolewa na DC- Mufindi Mheshimiwa Dkt.Linda Salekwa akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama siku ya kwanza ya ziara yake viwandani kuongea na wafanyakazi kuchukua kero na kusikiliza changamoto za Wawekezaji.
Amesema Majanga ya moto pindi yanapotokea Jeshi la zimamoto linatimiza wajibu wake lakini ni vyema kila kiwanda kiwe na akiba ya maji kwaajili ya majanga kama hayo pindi yanapotokea ili kuepusha moto usilete madhara makubwa
“ Hili ni agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mufindi, kujikinga na majanga ya moto yanayotokea mala kwa mala viwandani hii ni moja ya njia ya kujikinga na majanga hayo pindi yanapotokea. Mufindi ina viwanda vingi hebu tuchukue tahadhari”
“Rais wetu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Ni Balozi namba moja wa kuvuta wawekezaji nchini na kuweka mikakati ya kupunguza urasimu ili wawekeze katika mazingira Bora hivyo nipo hapa kusikiliza changamoto za wafanyakazi na changamoto za wawekezaji.” Lengo Ni kutoa huduma Bora kama Serikali na kuongeza mapato ya nchi kupitia wawekezaji hawa “
Jumla ya viwanda vinne vimetembelewa, kukaguliwa, kushauriwa na kuchukua changamoto za wafanyakazi ambavyo ni:-
Briquette Energy solution
QWIHAYA
SHEDA GENERAL
Mastern solution
Akizungumza Afisa Utekelezaji kutoka WCF Bi, Mariam Mlilapi amesema Taasisi yao inajukumu la kushughulikia mafao ya wafanyakazi wanapoumia au kupata Ajali wakiwa kazini ila Ni wajibu wa wamiliki wa Viwanda kuhakikisha wafanyakazi wao wote wanachangiwa katika mfuko wao ili kuepusha mtumishi kukosa haki zake pale anapopata majanga akiwa kazini.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi amepanga kuhakikisha Mufindi inakuwa Ni eneo sahihi kwa wawekezaji na Serikali inapata mapato yake kutoka katika viwanda hivyo. Aidha Mazingira ya Uwekezaji yanakuwa Salama na rafiki kwa wawekezaji kuwekeza na wafanyakazi wanafanya kazi bila kunyanyasika na wanapata haki zao kama wafanyakazi wengine nchini.
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.