Jumla ya vyandarua 80,540 vyenye viuatilifu vitagawiwa kuanzia leo tarehe 6/3/2023kwa wanafunzi wote wa Shule za Msingi 200 katika Wilaya ya Mufindi ambapo katika Halmashauri ya Mji Mafinga jumla ya shule Za Msingi 43 zitapewa vyandarua bila gharama yoyote kutoka Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI lengo likiwa ni kuhakikisha kiwango cha maralia kinapungua hadi kufikia asilimia sifuri(0%) ifikapo 2030.
Akizindua zoezi la ugawaji wa vyandarua katika Halmashauri ya Mji Mafinga,Shule ya Msingi Mkobwe Kata ya Boma yenye jumla ya wanafunzi 1100, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amesema kuwa Serikali kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ina lengo la kupunguza maralia kwa wananchi wake kufikia asilimia sifuri(0%)ifikapo 2030. Hivyo amewaomba wazazi na viongozi kusimamia matumizi sahihi ya vyandarua wananchi.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema lengo la Serikali ni kupunguza maralia nchini na shule zote 43 za Halmashauri ya Mji Mafinga wanafunzi watapewa vyandarua ambavyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 800.
Aidha Meneja MSD Mkoa wa Iringa Ndugu Robert Lugembe amesema kuwa vyandarua vitagawiwa bila malipo kwa wanafunzi wote wa shule za msingi ambapo jumla ya vyandarua 80,540 vitagawiwa vyenye viuatilifu ambapo Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa mitano ambayo imepokea vyandarua hivi chini ya Mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI kupitia MSD.Amesema kwa Wilaya ya Mufindi ugonjwa wa maralia ni chini ya asilimia (7.5%)hivyo lengo la Serikali ni kupunguza maralia ifikapo 2030 kufikia asilimia sifuri(0%)
Akitoa salamu kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema kama Serikali ngazi ya wilaya watahakikisha wananchi wanatumia vyandarua kwa lengo kusudiwa na matumizi sahihi na watoto wote wanalala kwenye vyandarua.
Uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu kwa wilaya ya Mufindi umehudhuriwa na wananchi na viongozi wa Chama na Serikali.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Halima Dendego
Angela Kairuki
Msemaji Mkuu wa Serikali
Wizara ya Afya (Health Ministry), Tanzania
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.