Nawaomba sana Sikilizeni vigezo vilivyowekwa vya kupata mikopo hii ya asilimia 10, umekosa awamu hii awamu ijayo hakikisha unapata kwa kufuata vigezo,tusiwe wabishi lazima tufuate vigezo ili tupate mikopo.
Fedha zinatolewa kila baada ya miezi mitatu kama umekosa awamu hii hakikisha unafuata vigezo na kuandika andiko vizuri ili upate mkopo kwa awamu inayofuata” DC- Mufindi Mheshimiwa Dkt Linda Salekwa.
Mhe. Linda amesema Serikali ipo kusimamia kila mwenye vigezo vya kupata mkopo anapata na kuhakikisha haki inatendeka kwa kila muombaji, wa Mikopo hii ya asilimia 10.
Amesema Lengo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Kuhakikisha mikopo inawanufaisha wananchi waliolengwa ili kuwainua kiuchumi,
“Naomba niwatoe hofu mikopo hii kwa awamu tunayotoa imepitiwa na kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya Ulinzi ya Wilaya , ile dhana ya kupeana mikopo haipo”
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa amechukua uamuzi wa kuwaita na kuwapa elimu wananchi wa Wilaya ya Mufindi waliokosa mkopo wa asilimia 10% ili kuwafafanulia vigezo vya mikopo ili awamu inayofuata waweze kupata mikopo hiyo isiyo na riba.
Sima Bingileki
Afisa Habari Mkuu- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.