Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita imefanya ziara katika Halmashauri ya Mji Mafinga kujifunza juu ya ukusanyaji wa mapato kupitia mazao ya misitu pamoja na vyanzo vingine.
Katika ziara hiyo ambayo imejumuisha wajumbe mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya, Mkurugenzi, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri , Madiwani, Wenyeviti wa vijiji ambao wamepewa elimu juu ya ukusanyaji wa mapato na kutunza misitu ambayo ndio chanzo cha mapato hayo.
Wajumbe hao wameelekezwa njia sahihi na ushirikiano mzuri na wananchi ili kuweza kukusanya mapato kwa usahihi na pia kuepuka migogoro ambayo inaweza kujitokeza katika shughuli iyo ya ukusanyaji wa mapato pia wameelekekezwa changamoto ambazo zinazo jitokeza katika ukusanyaji wa mapato ya mazao ya misitu na njia sahihi za utatuzi.
Aidha wamepewa mafunzo ya kuhakikisha misitu hiyo inalindwa kwa kufanya doria za mara kwa mara na pia kuibua fursa nyingine za misitu ikiwemo ufugaji wa nyuki ili kuhakikisha wanapata na kukusanya mapato ya mazao hayo kama vile asali ambazo zitaongeza mapato katika Halmashauri.
Michael Ngowi Afisa Habari
Wajumbe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chato kutoka Mkoa wa Geita wakiwa katika Halmashauri ya Mji Mafinga wakifatilia mafunzo ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu.
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.