Halmashauri ya Mji Mafinga imepokea kiasi cha shilingi 1,048,600,000/= kwaajili ya Utekelezaji wa Mradi wa Boost ambapo itajengwa Shule Mpya Moja yenye mkondo 1 Mwongozo Shule ya Msingi,Ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo katika Shule ya Msingi Gangilonga, Bumilayinga Shule ya Msingi Ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Mfano 2 Kwa Elimu ya Awali.
Mjimwema Shule ya Msingi Ujenzi wa vyumba vya madarasa 5 na matundu 3 ya vyoo.Shule ya Msingi Kinyanambo ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 4 ya vyoo. Shule ya Msingi Nyamalala ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo na Ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo katika Shule ya Msingi Sabasaba.
BOOST ni Mradi wa kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara BOOST ni sehemu ya Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo EP4R na inachangia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu kwa miaka mitano 2021/2022 hadi 2026.
Halmashauri ya Mji Mafinga inamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha katika Halmashauri ya Mji Mafinga hasa katika Sekta ya Elimu kupitia Mradi wa BOOST unaolenga kuboresha Miundombinu ya Shule.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.