HALMASHAURI YA MJI MAFINGA IMETOA MKOPO KWA VIKUNDI 27 WENYE THAMANI YA SHILINGI 276,700,000/= IKIWA NI ASILIMIA 10 YA MAPATO YA NDANI KWAAJILI YA KUVIWEZESHA VIKUNDI KIUCHUMI.
Akitoa taarifa ya Mikopo Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Happiness Laizer amesema kuwa vikundi vinavyopewa mikopo ni 27 ambapo vikundi 13 ni vya wanawake na wanakopeshwa shilingi 131,800,000/- Vijana vikundi 8 na wanakopeshwa shilingi 100,800,000/- na watu wenye Ulemavu Vikundi 6 wanakopeshwa shilingi 44,100,000/-
Naye Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Saad Mtambule amesema kuwa maombi ya mikopo yalikuwa ni bilioni 1 na wahitaji ni wengi hivyo wale waliopata mikopo kwa kukidhi vigezo basi wakaitumie mikopo vizuri na warejeshe ili kuwapa fursa na wengine kipindi kingine wakope.
“Wito wangu tukatumie fedha hizi vizuri asije akatokea mmoja wetu akapotea na hiyo pesa hatutakuacha hata kidogo, tutakusaka popote na sheri itachukua hatua,” Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule
Ameongeza kuwa wanufaika wa fedha hizi waseme wazi kwani ni mikopo inayotolewa na Rais kupitia Asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi Geirge Kavinuke amesema kuwa utoaji wa mikopo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inatoa mikopo isiyo na riba ii kuwainua wananchi Kiuchumi.
“Lazima Mikopo hiyo irejeshwe kwasababu ipo kisheria na msiporejesha hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote watakaochezea mikopo hii au kushindwa kurejesha,” Mwenyekiti wa CCM Mufindi Kavinuke.
IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SEIKALINI-MAFINGATC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.