SERIKALI KATIKA KUHAKIKISHA KILA MWANAFUNZI ANAPATA ELIMU YA MSINGI KATIKA MAZINGIRA BORA INAJENGA SHULE MPYA YA MSINGI JJMUNGAI KUPITIA MPANGO WA BOOST MILIONI 326.5- MAFINGA
Akizungumza Afisa Elimu Awali na Msingi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Dorothy Kobelo amesema kuwa shule inayojengwa niya Mkondo Mmoja ambayo itakuwa na Madarasa 2 ya Awali na Matundu 6 ya vyoo kwa Wavulana na Matundu 3 na Wasichana Matundu 3 pia Yanajengwa Madarasa 6 ya Wanafunzi ambayo yatakuwa na Matundu ya Vyoo 10 kwa Wavulana Matundu 5 na Wasichana Matundu 5.Fedha zinazotumika katika Ujenzi wa Shule ya JJ.Mungai ni Shilingi Milioni 326,500,000 kutoka Serikali Kuu kupitia Mpango ws BOOST.
Amesema ujenzi umefikia hatua ya kuezeka ambapo inajengwa Shule ya Msingi na Awali ambapo ikikamilika itaweza kupokea wanafunzi kwa mwaka 2026.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Fidelica Myovella akiwa katika ziara ya ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo amesema kuwa fedha zilizopokelewa kwaajili ya PROGRAMU YA BOOST( Awamu ya Tatu)
ni kwaajili ya Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi JJ MUNGAI 326,500,000 /-na
Shule ya Msingi Lumwago imepokea Kiasi cha Shilingi 112,000,000 /- kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa 4 na matundu 6 ya vyoo pamoja na mapokezi ya shilingi Milioni 69.1 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 2 ya mfano ya Awali na matundu 6 ya vyoo vya Awali.
“ Tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuleta fedha kwenye sekta mbalimbali katika Halmashauri yetu ya Mji Mafinga. Ujenzi wa Shule hii mpya ya Msingi umefikia hatua ya kuezeka na kwakuwa kila kitu kipo site tunategemea ukamilishaji wa ujenzi utakuwa wa ubora na thamani ya fedha iliyowekwa itaendana na ubora wa Majengo”
BOOST ni programu yenye lengo la kuboresha upatikanaji fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara ambayo ni sehemu ya mpango wa lipa kulingana na Matokea katika Elimu.
Imeandaliwa na
Sima Mark Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.