HALMASHAURI YA MJI MAFINGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA TACTIC
Posted on: May 9th, 2025
Halmashauri ya Mji Mafinga ni moja kati ya Halmashauri 18 nchini zitakazonufaika na Mradi wa TACTIC kwa Awamu ya Tatu, ambapo Wataalamu Washauri kutoka TACTIC wamepokea maoni ya Wadau mbalimbali wa MJI Mafinga baada ya kuwasilisha michoro ambayo ni matokeo ya kufanya upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina wa Mradi wa UJenzi wa Stendi ya Kisasa ya Mabasi Eneo la Kinyanambo na Utengeneaji Wa Barabara kwa kiwango cha lami katika Maeneo mbalimbali ya Mji Mafinga.
Timu ya Wataalamu kutoka OR- TAMISEMI kwenye Mradi wa TACTIC wakiongozwa na Mtaalamu Mshauri Mhandisi Umit Giris kutoka Kampuni Binafsi ya BOTEK Tech Consulting wamewasilisha Michoro ya Miradi hiyo kwa Timu ya Menejimenti na Wadau kutoka TARURA na POLISI ili kupokea Maoni baada ya Wataalamu hao kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Maeneo ambapo Miradi hiyo Itatekelezwa.
Aidha Wadau na Wataalamu wametoa maoni kulingana na wasilisho la Wataalamu hao washauri na kuahidi kuyafanyia kazi kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa Miradi hiyo.
Wataalamu hao washauri wamepokelewa na Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella akiwa na Timu ya Menejimenti na Mhandisi Joseph Temba ambaye ni Mratibu wa Miradi ya TACTIC katika Halmashauri ya MJI Mafinga.
TACTIC ni Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania na Moja ya Malengo ya Miradi ya TACTIC ni kugusa wananchi wengi na Wananchi wa hali za kawaida, kuinua uchumi na kuboresha uwezo wa Taasisi katika Kutoa huduma bora kwa wananchi.
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Mafinga TC