Halmashauri ya Mji Mafinga yaanza rasmi tarehe 14/3/2023 kutoa leseni za Biashara kwa Mfumo wa Tausi.
Akizungumza Ndugu Charles Tuyi Mkuu wa Kitengo cha Usafi wa Mazingira na Udhibiti wa taka kwaniaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Happiness Laizer amesema kuwa mfumo huu wa TAUSI utasaidia kuondoa msongamano kwenye Ofisi Ya Biashara kwani Mfanyabiashara atajihudumia mwenyewe eneo alipo na akikidhi vigezo atapokea Hati ya malipo na kulipia ili kupata leseni ya biashara.
Aidha amewataka wananchi kuchangamkia fursa hii kwani Serikali imerahisisha utoaji huu wa huduma ya leseni ya biashara kwa njia ya mtandao.
Aidha Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara na Halmashauri ya Mji Mafinga Ndugu, Evance Mtikile amesema Mfumo huu wa Utoaji wa Leseni kwa njia ya Mtandao Utarahisisha Utoaji wa Leseni na Ni rahisi kwa mfanyabiashara huko aliko anaweza kupata leseni akishakamilisha taratibu zote zinazomtaka akiwa kwenye Mfumo wa TAUSI.
Amesisitiza kuwa Divisheni ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Umenipanga kuwafikia wafanya biashara wote ndani ya Mji Mafinga ili kila mwananchi anayestahili kupata leseni apate na kwa wakati.
Akiishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanziasha Mfumo huu Mmiliki wa KAMPUNI ya JANAKI VETERINARY CENTER amesema kuwa mfumo wa TAUSI utasaidia sana kupunguza foleni katika Ofisi za Utoaji wa Leseni na itamsaidia mfanyabiashara kupata leseni mapema alipo na kwa wakati ikiwa tu umetimiza vigezo kwa kuingia kwenye Mfumo na kuwa na viambatanishi vinavyohitajika.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-MAFINGA TC
Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Mafinga TC
@ortamisemi
@maelezonews
@salekwalinda
Halima Dendego
Angel Kairuki
Msemaji Mkuu wa Serikali
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.