Halmashauri ya Mji Mafinga imepata Hati Safi ya Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2022 kulingana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG)
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amesema kuwa Mafanikio haya ya Kupata Hati Safi yametokana na Ushirikiano mzuri baina ya Waheshimiwa Madiwani kusimamia Halmashauri vizuri, Wataalamu kutimiza wajibu wao na Mkaguzi wa Ndani kushauri kimkakati.
“ Niwapongeze Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kwa kupata Hati Safi, lakini kipekee kati ya Halmashauri zote, hii ya Mafinga TC imekuwa na hoja chache kuliko Halmashauri nyingine, ili kuepukana na Hoja hakikisheni mnasimamia matumizi ya Fedha kwa kufuata sheria, Kanuni na Taratibu. Mji fanya
Hivyo hamtakuwa na Hoja za Ukaguzi
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amewataka Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga kuifahamu Miradi inayotekelezwa kwenye Kata zao, thamani ya Mradi na muda wa Utekelezaji wa Mradi hiyo ili kuepukana na Hoja za Ukaguzi kwa kusimamia ipasavyo Miradi hiyo.
Akizungumza katika Mkutano huo wa Baraza la Madiwani la kujadili majibu ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha unaoishia tarehe 30 Juni 2022 Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Mhandisi Learnad Masanja amewataka Wataalamu kufanya kazi kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani kwani wao ndo wenye Halmashauri na kwa kufanya hivi itapunguza sana hoja kwani ushirikiano utakuwepo na Miradi itasimamiwa kwa kufuata Sheria na kanuni.
Baraza limehudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ngazi ya Mkoa na Wilaya, wakaguzi wa nje ngazi ya Mkoa, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wataalamu Halmashauri ya Mji Mafinga wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mji ndugu, Ayoub Kambi
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA TC
Sima Bingileki
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mafinga TC
Mafinga Town.
Postal Address: Po.Box 76 Mafinga
Simu: +255 262 772 393
Mobile: 026-2772393
Barua Pepe: td@mafingatc.go.tz
Copyright ©2018 Mafinga Town Council . All rights reserved.